TAARIFA YA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI HALMASHAURI YA MANISPAA MPANDA - TASAF III KUANZIA APRILI 2014 HADI APRILI 2018:
1:0 UTANGULIZI:
Awamu ya tatu ya Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF III) inayotekeleza Mpango wa kunusuru kaya maskini ilizinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mwezi Agosti mwaka 2012.Katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda mpango huu ulizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi mhe. Dk. Rajabu Rutengwe mnamo tarehe 8, Aprili 2014 katika ukumbi wa Idara ya Maji Halmashauri ya Wilaya Mpanda, ambapo ilifuatiwa na Warsha Maalum kwa Wadau wote wa Mpango huu katika Halmashauri ya Mji na kuongozwa na Timu kutoka TASAF Makao Makuu (TMU).
Kupata taarifa zaidi juu ya tasaf katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda bonyeza hapa TAARIFA YA TASAF 2018.pdf
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.