• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mpanda Municipal Council
Mpanda Municipal Council

Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa Mpanda

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mission and Vission
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Ujenzi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
        • Tasaf
      • Fedha na Biashara
      • Usafishaji na Mazingira
      • Mipango, Takwimu, Uchumi na Tathmini
      • Land and Town Planning
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Kitengo cha Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha TEHAMA na Mahusiano ya Umma
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Uchaguzi
    • Muundo wa Taasisi
    • Kata
    • Streets
  • Fursa za uwezekezaji
    • Vituo vya Utalii
    • Sekta ya Madini
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Uvuvi
    • Sekta ya Kilimo
    • Sekta ya ufugaji
  • Huduma zetu
    • Elimu
      • Rungwa Sekondari
      • Mpanda Girls Sec School
    • Heath
    • Usafi na Mazingira
    • Maji
    • Ardhi na Maliasili
    • Ujenzi na Miundombinu
    • Woman Empowerment
  • Madiwani
    • List of Counciolors
    • Standing Commitees
    • Time table
      • Vikao vya Madiwani
    • Makablasha/Taarifa za Baraza
  • Miradi
    • Miradi inayo tekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • By laws
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Strategic Plan
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi
    • Speech
    • Albamu
    • Makala

WASINDIKAJI WAWEZESHWA MIUNDOMBINU NA MASHINE

Posted on: November 16th, 2022

WASINDIKAJI WAWESHWA MIUNDOMBINU NA MASHINE

Bi Cresensia Joseph kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko amefungua rasmi jengo la wasindikaji wa bidhaa mbalimbali lilopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda lililojengwa chini ya mradi wa Kilimo Bora cha Mboga na Matunda kwa Wanawake na Vijana KIBOWAVI chini ya AGRI - CONNECT linalofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU). Ufunguzi wa jingo hilo umefanyika 16 Novemba 2022.

Akiwasilisha taarifa ya ujenzi na ununuzi wa mashine za viliyogarimu zaidi ya milioni 200  afisa maendeleo ya jamii Bi Maritha Mlozi alieleza kuwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa kushirikiana na Umoja wa Wasindikaji wa Mboga na Matunda (UWAMBOMAKA) iliwasilisha ombi la uwezeshwaji katika maeneo ya kuboresha majengo, mafunzo na vifaa kwa ajili ya shughuli za uzalishaji na usindikaji, kwenda mradi wa Kilimo Bora cha Mboga na Matunda kwa Wanawake na Vijana (KIBOWAVI) chini ya AGRI – CONNECT linalofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU). Hii ilitokana na changamoto walizokuwa wanapitia wasindikaji kutokana na kusindika kienyeji bidhaa mbalimbali za chakula majumbani ambako mazingira yalikuwa siyo rafiki kiafya na kutoruhusu wasindikaji kupata nembo za ubora (TBS).

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda bi Sophia Kumbuli amemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutafuta wafadhili ambao wamewezesha ujenzi na ukarabati nua ununuzi wa mashine mbalimbali ambazo zitarahisisha na kuongeza thamani na uzalishaji katika shughuli za wajasiliamali.

Akiwasilisha hotuba ya mkuu wa mkoa wa katavi Bi Cresensia Joseph kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa katavi amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuilinda miundombinu, mashine  na kuendeleza yote ambayo ya yamejengwa katika kiwanda ambacho kimezinduliwa.

“Kujengewa miundombinu, kununua mashine na kupewa mafunzo ni jambo moja, jambo lililopo mbele yetu ni kuhakikisha yote yaliyoanzishwa na kufadhiliwa na wafadhili yanaendelea, kwa kweli sitegemei kukuta kiwanda hiki kilichosheheni mitambo kimetelekezwa na hakifanyi kazi.” Alisema Bi Cresensia Joseph kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Katavi

Aidha  Bi Sophia amemshukuru sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta wafaddhili, pia amelishukuru shirika la HELVETAS - TANZANIA kupitia mradi wa KIBOWAVI chini ya AGRI - CONNECT linalofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kuwawezesha wajasiriamali kuwapatia mafunzo, vifaa, mashine na kuwaboresha mazingira ya usindikaji, uwezeshaji huu utaongeza thamani wa bidhaa, utaboresha masoko na hivyo kuwaongezea kipato.

“Tunamshuru sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea wafadhili, pia Tunalishukuru sana shirika la HELVETAS - TANZANIA kupitia mradi wa KIBOWAVI chini ya AGRI - CONNECT linalofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) ambao wametufadhili ujenzi wa majengo mapya na ukarabati wa majengo ya zamani kama yafuatayo; Duka la kuuzia (Supermarket),Jengo la kutengenezea juice na matunda, Jiko, Vyumba 2 vya kubadilishia nguo, Vyoo 2, Mtambo wa kusindika Wine, Mashine za kusagia unga wa lishe na viungo, Chumba cha kusagia, Mashine ya kukata viungo, Freezer 2, Mfumo wa umeme wa jua, Uzio, Kaushio (solar drier), Shelves, CCTV CAMERA 15 ambavyo vyote kwa pamoja vimegharimu zaidi ya shilingi milioni 200” . Alisema Maritha Mlozi kwa niaba ya Mkurugenzi

Bi Sophia amemuhakikishia mwakiliahi wa Mkuu Mkoa wa Katavi kuwa Manispaa ya Mpanda itailinda miundombinu yote iliyojengwa na mashine zote zilizonunuliwa kwa ajili ya kuwawezesha wasindikaji. Aidha Manispaa itaendelea kushirikiana na Umoja wa Wasindikaji wa Mboga na Matunda (UWAMBOMAKA) pamoja na wadau wote ili kuhakiksha tija ya kiwanda iliyokusudiwa inapatiaka.

 

 

Matangazo

  • MWALIKO WA KOTESHENI YA ZABUNI YA KUENDESHA MGAHAWA April 21, 2022
  • ORODHA YA WALICHAGULIWA KUFANYA KAZI YA ANUANI ZA MAKAZI March 28, 2022
  • KUITWA KWENYE MAFUNZO YA SENSA July 28, 2022
  • FOMU YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA KWA SHULE ZA MANISPAA YA MPANDA December 01, 2021
  • Tazama zote..

Habari za Hivi Punde

  • MANISPAA YA MPANDA YAKABIDHI MADARASA 51

    December 28, 2022
  • WASINDIKAJI WAWEZESHWA MIUNDOMBINU NA MASHINE

    November 16, 2022
  • RC KATAVI ARIDHISHWA NA UJENZI WA MADARASA MPANDA

    November 09, 2022
  • SENDIGA AKOSHWA NA HATUA ZA UJENZI WA MADARASA MANISPAA YA MPANDA

    October 25, 2022
  • Tazama zote..

Video

Uzinduzi wa Tovuti mpya kitaifa
Video zaidi.

Kurasa za Haraka

  • Revenue Collection Dashboard for Katavi Region

Tovuti Zinazohusiana

  • TAMISEMI
  • Utumishi wa Umma
  • Tovuti ya Ajira
  • Tovuti kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

professional Writing Service

Ramani

Wasiliana Nasi

    Ilembo, Kasimba area

    Anuani ya Posta: 216, Mpanda

    Simu ya Mezani: +255-2529529

    Simu: +255-2529529

    Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.