Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf akiambatana na watumishi wa ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda amekabidhi zawadi mbalimbali kwa niaba ya Mwenge wa Uhuru 2023 kwa mama aliyejifungua Agosti 25, 2023 katika kituo cha afya Kazima.
Mama huyo Anastazia Laurent amepata bahati hiyo ya kihistoria baada ya kujifungua mtoto wa kiume aliyempa jina la Mwenge kitendo kilichomkosha Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Abdallah Shaib Kaim na kuahidi kumpa zawadi kama motisha kwa kitendo chake cha kizalendo na kuuenzi mwenge wa uhuru.
Hiyo ilijikuwa ni Agosti 25, 2023 wakati Mwenge wa uhuru ulipofika katika kituo cha afya Kazima kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo hicho kama moja ya miradi iliyofikiwa na Mwenge kwa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.
'Mama Mwenge' mkazi wa mtaa wa Kazima mjini Mpanda, hajasita kuonesha furaha yake huku akijivunia uamuzi wake wa kumpa mwanae jina hilo na kueleza kuwa tukio hilo litaendelea kusalia kama alama ya uzalendo katika maisha yake.
DC Jamila amekabidhi zawadi mbalimbali ikiwemo doti za vitenge na pesa taslimu
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.