Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuf leo Agosti 31, 2023 amefanya ziara ya kutembelea mradi wa ukarabati na ujenzi wa majengo mapya katika Hospitali ya manispaa ya Mpanda.
Akiingoza kamati ya Usalama ya wilaya ya Mpanda DC Jamila ameonesha kuridhishwa na ujenzi wa mrandi huo huku akimuagiza mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda kuhakikisha anasimamia kukamilika ujenzi wa mradi huo ifikapo Oktoba 30, 2023.
"Kwa kuona kwa macho tumeridhika na kazi ambayo imefanywa hapa chini ya usimamizi wa wataalamu wetu, bado sehemu chache ambazo bado zinaendelea na ukamilishaji ikiwepo kuwekea vitu kama milango na maeneo machache ambayo yamebaki kwa ajili ya ukamilishaji ili hospitali iweze kukamilika kabisa" Jamila Yusuf, DC Mpanda.
Amewataka watumishi wa Idara ya afya katika manispaa ya Mpanda kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya ili kuondoa malalamiko kwa wananchi wanaowahudumia
"Wananchi watakapofika na kukuta majengo haya yamekamilika na kupendeza basi na huduma zetu na zenyewe ziwe ni huduma zinazorudisha matumaini, lugha iwe ni nzuri, atakapofika mtu kupata huduma hapa akikutana na mtumishi kwa kweli apate matumaini ya kuendelea kuishi na sisi tuna imani na wanaotoa huduma katika wilya yetu ya Mpanda" aliongeza DC Jamila.
Mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 869.5 umejumuisha ukarabati wa majengo 9 na ujenzi wa majengo mapya manne huku jengo moja likimaliziwa ambapo kwa mujibu wa Mganga mkuu wa Hospitali hiyo Dokta Lugatha Paul karabati huo umelenga kuboresha huduma kwa wakazi wa manispaa ya Mpanda.
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.