Historia fupi ya Manispaa ya Mpanda
1.0 Utangulizi
Halmashauri ya Manispaa Mpanda ilianza kama Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpanda tarehe 1 Julai, 1990 kwa mujibu wa gazeti la Serikali Namba 137 la tarehe 8, Juni, 1990. Aidha tarehe 1 Julai, 2003 Hati ya kuanzishwa rasmi kwa Mamlaka ya Mji Mdogo ilitolewa na Halmashauri mama (Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda). Miaka miwili baadaye Serikali kupitia gazeti la Serikali Namba 218 la tarehe 29 Julai, 2005 ilitangaza nia ya kuanzishwa kwa Halmashauri ya Mji wa Mpanda. Hivyo, Serikali ilitangaza kuanzishwa rasmi kwa Halmashauri ya Mji wa Mpanda tarehe 1 Julai, 2007 kupitia tangazo la Serikali Namba 136 la tarehe 29 Septemba 2006. Halmashauri hii ni miongoni mwa Halmashauri mpya 13 zilizoanzishwa rasmi katika mwaka wa fedha 2007/2008, na kujitenga kutoka kwenye Halmashauri zao za awali. Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ilitangazwa rasmi tarehe 01, Julai 2015 kupitia tangazo la Serikali Namba 220
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ni kati ya Halmashauri 5 zilizomo ndani ya Mkoa wa Katavi. Iko upande wa magharibi mwa Tanzania, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ipo katikati ya mkoa wa Katavi katika safu za miinuko ya Katumba miongoni mwa kanda 5 za kilimo za Mkoa huu waKatavi. Manispaa inapatikana kati ya latitude 5o 15’ na 7o 3’ na 15-30 kusini mwa ikweta na longitude 30o 31 na 33o00 mashariki mwa Ikweta. Kwa upande wa kaskazini inapakana na Halmashauri ya Wilaya, Mashariki inapakana na Halmashauri ya Nsimbo
1.2 Hali ya Kijiografia
Manispaa ya Mpanda ina hali ya hewa ya joto la kati kwa sehemu kubwa kwa mwaka. Wastani wa joto kwa mwaka ni nyuzi joto 29, Hali ya hewa ya baridi inaanza mwezi wa Juni hadi Julai ikiwa na hali ya baridi ya nyuzi joto 7. Mvua huanza mwezi wa Novemba na huisha mwishoni mwa mwezi wa Aprili. Wastani wa mvua ni mm 1000 hadi 1200 kwa mwaka, ambazo huambatana na radi na ngurumo za hapa na pale
Manispaa ya Mpanda ina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba of 527 ambapo kati ya eneo hilo kilomita za mraba 30 ni sehemu ya Maji. Kiutawala Manispaa ina tarafa 02 kata 15 mitaa 43, vijiji 14 na Vitongoji 78.
1.6 Idadi Ya Watu
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya Agosti, 2012 wakazi wa eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda ni 118,150. Kati yao wanaume ni 58,116, wanawake ni 60,034. Ongezeko la watu ni 3.6 asilimia kwa mwaka na ina jumla ya kaya 24,275, ikiwa ni wastani wa watu 4.9 kwa kaya. Kwa sasa (2018) Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda inakadiriwa kuwa na watu wapatao 146,081 ambapo wanaume ni 71,855 na wanawake ni 74,226 na Kaya 30,014
Ilembo, Kasimba area
Anuani ya Posta: 216, Mpanda
Simu ya Mezani: +255-2529529
Simu: +255-2529529
Barua Pepe: md@mpandamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa Mpanda. Haki Zote Zimehifadhiwa.